1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMadagascar

Rajoelina aidhinishwa mshindi wa uchaguzi Madagascar

2 Desemba 2023

Mahakama Kuu ya Katiba nchini Madagascar imesema rais wa sasa wa nchi hiyo Andriy Rajoelina ndiye mshindi wa uchaguzi uliofanyika Novemba 16.

Andry Rajoelina achaguliwa kwa muhula wa pili wa urais Madagascar
Andry Rajoelina achaguliwa kwa muhula wa pili wa urais Madagascar Picha: Lewis Joly/REUTERS

Mahakama Kuu ya Katiba nchini Madagascar imesema rais wa sasa wa nchi hiyo Andriy Rajoelina ndiye mshindi wa uchaguzi uliofanyika Novemba 16. Rajoelina ametangazwa ushindi baada ya kupata asilimia 58.96 ya kura zote zilizopigwa.

Mahakama hiyo imetupilia mbali kesi zilizokuwa zimewasilishwa mbele yake kuupinga ushindi wake. Mojawapo ya pingamizi zilizokuwa zimewasilishwa lilitoka kwa mmoja wa washindani wake wakuu,  wakili Siteny Randrianasoloniaiko.

Wagombea 10 kati ya 13 waliokuwa wamejiandikisha kuwania urais, waliususia uchaguzi huo ingawa majina yao tayari yalikuwa katika makaratasi ya kupigia kura.

Kabla kufanyika uchaguzi huo, kulishuhudiwa maandamano ya wiki kadhaa huku upinzani ukisema Rajoelina aliweka mazingira ya uchaguzi ya upendeleo na waliojitokeza kushiriki zoezi hilo walikuwa chini ya asilimia 50 ya wapiga kura.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW