Rajoelina amteua Waziri Mkuu mpya mwanajeshi
7 Oktoba 2025
Matangazo
Akizungumza akiwa ikulu, Rajoelina alisema waziri Mkuu mpya anapaswa "kuwahudumia wananchi" na awe "mtu safi, mwenye uadilifu, na anayefanya kazi kwa haraka." Pamoja na kiongozi huyo kutoa ahadi ya kile alichokiita "tayari kuiokoa Madagascar", hatua yake ya kuvunja serikali nzima wiki iliyopita haikuweza kukidhi kiu ya waandamanaji.Maandamano hayo, ambayo yalianza kutokana na hasira dhidi ya kukatika kwa maji na umeme mara kwa mara katika kisiwa hicho cha Bahari ya Hindi chenye umasikini, yamegeuka kuwa harakati za kupinga serikali zinazomtaka Rajoelina ajiuzulu.