1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH : Abbas amesema anadhibiti Gaza

16 Septemba 2005

Rais Mahmoud Abbas wa Palestina amesema serikali yake ina udhibiti kamili wa Ukanda wa Gaza.

Kauli yake hiyo inakuja licha ya ukweli kwamba mamia ya watu kwa mara nyengine tena wamevuka mpaka kati ya Gaza na Misri.Wakati huo huo kundi la wabunge wa Kipalestina limewasilisha hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Ahmed Qorei.Wanailamu serikali yake kwa kuongeza vurugu kufuatia kujitowa kwa Israel kwenye Ukanda wa Gaza mapema wiki hii.

Na katika Mkutano wa Kilele wa Umoja wa Mataifa mjini New York Waziri Mkuu wa Israel Ariel Sharon amesema hatua inayofuata katika mchakato wa amani wa Mashariki ya Kati inategemea Wapalestina wenyewe.Sharon amesema kujitowa kwa Israel kwenye Ukanda wa Gaza kumefunguwa fursa ya kuundeleza mpango wa amani unaojulikana kama ramani ya amani.