1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH. Abbas amlaumu Sharon kwa kumdunisha.

13 Aprili 2005

Rais wa Palestina, Mahmaoud Abbas amemlaumu waziri mkuu wa Israel, Ariel Sharon, kwa kujaribu kumudunisha katika mkutano wa kilele kati ya Sharon na rais George W Bush wa Marekani huko Texas. Abbas amesema alishangazwa na kampeni ya Sharon dhidi ya mamlaka ya Palestina katika mkutano huo. Vyombo vya habari nchini Israel vilitangaza kwamba Sharon aliwaambia wamarekani kwamba Abbas anafanya juhudi za kuendelea kubakia madarakani. Sharon alimtaja Abbas kama mwenyekiti wa mamlaka ya Palestina na wala sio rais, huku rais Bush akimtaja kama rais wa Palestina.