1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH: Chama cha Hamas kinasema hakitoitambua Israel

15 Novemba 2006

Chama tawala cha Kipalestina Hamas kimesema,hata baada ya serikali ya umoja kushika madaraka, chama hicho hakitoitambua Israel au kukubali ufumbuzi wa kuwa na madola mawili kuhusu mgogoro wa Mashariki ya Kati.Msimamo huo huenda ukavuruga juhudi za kuunda serikali ya wastani na kufungua njia ya kupata msaada muhimu wa kigeni.Marekani na washirika wake katika kundi la pande nne la wasuluhishi wa mzozo wa Mashariki ya kati wamesita kutoa misaada ili kuishinikiza Hamas kutambua haki ya kuwepo kwa taifa la Israel, kukanusha matumizi ya nguvu na kukubali mikataba ya amani pamoja na Israel ilioko hivi sasa. Wafadhili wa utaratibu wa amani wa Mashariki ya Kati wanataraji kukutana leo hii mjini Cairo kujadili juhudi za kufufua majadiliano,kati ya Waisraeli na Wapalestina.