1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH: Fursa ya kufufua majadiliano yaliyokwama

6 Novemba 2007

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani,Condoleezza Rice amekutana na Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas mjini Ramallah.Baadae kwenye mkutano pamoja na waandishi wa habari Rice alisema,mkutano wa amani wa Mashariki ya Kati uliopangwa kufanywa nchini Marekani,utatoa fursa halisi ya kuanzisha upya majadiliano kati ya Israel na Wapalestina ambayo yamekwama tangu muda mrefu.

Mkutano wa amani wa Mashariki ya Kati unaosimamiwa na Marekani unatazamiwa kufanywa mwishoni mwa mwezi huu Novemba au mapema Desemba mjini Annapolis,Maryland nchini Marekani.