RAMALLAH: Hamas na Fatah wajadiliana kuunda serikali ya umoja
13 Novemba 2006Matangazo
Chama tawala cha Wapalestina Hamas na Fatah cha rais Mahmoud Abbas,vimeendelea na majadiliano ya kuunda serikali ya umoja wa taifa.Ripoti zilizosema kuwa pande hizo mbili zimekubaliana nani atakaekuwa waziri mkuu mpya,bado hazijathibitishwa.Vyama hivyo vinatumai,hatua ya kuunda serikali ya umoja,itasaidia kuzishawishi Marekani na nchi za Umoja wa Ulaya kuregeza vikwazo vya misaada.Nchi za magahribi ziliweka vikwazo hivyo baada ya Hamas kukishinda chama cha Fatah katika uchaguzi wa mwezi Januari.Marekani na Umoja wa Ulaya zinaitaka serikali ya Wapalestina iitambue Israel na itangaze kuacha matumizi ya nguvu.