1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ramallah. Kiongozi wa Palestina akutana na kiongozi wa wabunge.

27 Agosti 2005

Kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas amekuwa na mazungumzo leo na kiongozi wa kundi la chama cha mrengo wa kushoto kati cha Labour katika bunge la Israel, Efraim Sneh.

Viongozi hao wawili wamejadiliana kuhusu mpango uliokamilika hivi karibuni wa kuwaondoa walowezi wa Kiyahudi kutoka eneo la ukanda wa Gaza pamoja na makaazi manne ya ukingo wa magharibi , na jinsi ya kuwezesha kurejesha mpango wa amani ya mashariki ya kati uliokwama katika njia yake.

Wapalestina na jumuiya ya kimataifa inasisitiza hatua za haraka katika kurejea tena katika mpango wa amani mara baada ya Israel kukamilisha kujiondoa kutoka Gaza.

Uondoaji wa walowezi wa Kiyahudi wapatao zaidi ya 8,000 ulikamilika mapema mwezi huu, na majeshi yanatarajia kukamilisha kuondoa kutoka katika maeneo hayo ifikapo katikati ya mwezi wa Septemba.