1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH: Kwa mujibu wa waziri wa mambo ya kigeni NABIL SHAATH,...

9 Desemba 2003
serikali ya Wapalastina inajitahidi zaidi hadi upatikane muwafaka wa kusitisha mapigano Mashariki ya Kati. Aliliambia shirika la habari Reuters kuwa, kwa jumla kuna utayarifu wa kusimamisha mapigano hayo. Mazungumzo ya makundi ya wapalastina yaliharibika mjini Cairo Jumaapili iliopita. Vyama vya washupavu Hamas na Jihad viko tayari pekee kutowahujumu raia nchini Israel. Chama Hamas kimetangaza kutakuwapo hujuma za kujitolea mhanga kufuatia kuvunjika kwa mazungumzo hayo.