Ramallah: Mapambano baina ya Rais Abbas wa Palestina na serekali ya Chama cha Hamas.
6 Juni 2006Makombora yaliofyetuliwa kutoka roketi yalielekezwa katika makao makuu ya Idara ya Usalama inayodhibitiwa na chama cha fatah cha Wapalastina, hivyo kuwajeruhi si chini ya watu watatu. Idara hiyo ni tiifu kwa Rais Mahmud Abbas wa Palastina na imekuwa katikati kwenye mapambano ya madaraka baina ya Bwana Abbas na chama cha siasa kali cha Hamas kinachotawala. Shambulio hilo la leo limekuja wakati Rais Abbas amekipa Chama cha Hamas siku tatu zaidi kuikubali hati ambayo kichinichini inaitambua dola ya Israel, ama sivyo ataliwasilisha jambo hilo mbele ya wananchi kwenye kura ya maoni. Wito wa Mahmud Abbas kutaka iitishwe kura ya maoni umeungwa mkono na viongozi wa Chama cha Ukombozi wa Palastina, PLO, lakini tarehe ya kufanyika kura hiyo bado haijawekwa.