1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH Mateka waachiliwa huru huko Gaza

14 Julai 2005

Mateka wa Uingereza na Austria waliotekwa nyara nchini Palestina wameachiliwa huru. Maofisa wa Palestina wametangaza kuachiliwa huru kwa wahandisi hao waliokuwa wametekwa nyara katika kambi moja huko Gaza. Wakaazi wa kambi hiyo wanasema wanaume hao waliokuwa wakifanya kazi kwenye mradi wa maji, walitekwa nyara walipokuwa ndani ya motokaa yao na watu waliokuwa wamejifunika nyuso zao. Watekaji nyara hao walitaka kuishinikiza mamlaka ya Palestina kuwaachilia huru jamaa zao wanaotumikia vifungo garezani.