1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH: Matumaini ya kuachiliwa mwanajeshi wa Kiisraeli

28 Julai 2006

Rais wa Wapalestina,Mahmoud Abbas amesema anaamini kuwa mwanajeshi wa Kiisraeli alietekwa nyara mwezi uliopita kwenye mpaka wa Gaza huenda akaachiliwa huru hivi karibuni.Abbas,akizungumza mjini Rome alikokwenda kukutana na waziri mkuu wa Italia Romano Prodi,alisema hatua zinachukuliwa kupata uhuru wa mwanajeshi huyo.Lakini madai hayo yamekanushwa na tawi la kijeshi la Hamas, lililomteka nyara mwanajeshi huyo wa Israel. Msemaji wa kundi hilo amesema,Rais Abbas hana mamlaka ya kuamua ikiwa koplo huyo wa Kiisraeli aachiliwe huru.