1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ramallah. Mlowezi mmoja wa Kiyahudi auwawa katika ukingo wa magharibi.

25 Juni 2005

Majeshi ya Israel yamewakamata wapiganaji 14 wa Islamic Jihad leo Jumamosi katika eneo la ukingo wa magharibi muda mchache baada ya watu wenye silaha kumuua mlowezi mmoja wa Kiyahudi, wakati makubaliano tete ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Palestina yakionekana kuporomoka zaidi.

Israel katika muda wa siku chache zilizopita wamewakamata watuhumiwa 63 wa kundi la Islamic Jihad katika eneo la ukingo wa magharibi na kuanza tena sera za kuwauwa viongozi wa kundi hilo, wakati wapiganaji hao walipomuua mlowezi mwingine wa Kiyahudi hapo siku ya Jumatatu. Hakuna kundi lililodai kuhusika na mauaji ya mlowezi huyo wa Kiyahudi jana Ijumaa.