1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH: Mwito wa kuanzisha majadiliano ya amani

4 Septemba 2005

Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas amesema majadiliano ya amani ya Mashariki ya Kati yapaswa kuanzishwa mara tu ya Israel kukamilisha utaratibu wa kuhama Gaza.Rais Abbas amesema ni matumainio yake kuwa taifa la Palestina litaundwa hadi mwakani.Katika mahojiano yake na Shirika la habari la Associated Press,Abbas vile vile aliahidi kuwa katika muda wa wiki tatu zijazo,atayadhibiti na kuyaleta pamoja makundi mbali mbali ya wanamgambo wa chama tawala cha Fatah.Amesema kwamba Marekani imemuhakikishia kuwa majadiliano ya amani pamoja na Israel yanaweza kuanzishwa tena,Israel itakapomaliza tu mpango wake wa kuhama Gaza.Inatazamiwa kuwa hadi Septemba 15 Israel itakamilisha utaratibu wa kuhama.