1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ramallah. Palestina kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

12 Septemba 2006

Baada ya miezi kadha ya majadiliano, rais wa Palestina Mahmoud Abbas amesema kuwa amefikia makubaliano na waziri mkuu Ismail Haniyeh wa chama cha Hamas kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Lakini kundi la Hamas limeshindwa kutimiza masharti ya mataifa ya magharibi ya kuachana na matumizi ya nguvu.

Hii inazusha maswali juu ya iwapo serikali ya umoja wa kitaifa itaridhisha madai ya mataifa hayo ya magharibi ili kuweza kuondoa vikwazo vilivyowekwa baada ya chama cha Hamas kuchukua madaraka mwezi wa March.

Msaidizi wa Abbas amesema kuwa serikali iliyopo madarakani ya chama cha Hamas itavunjwa katika muda wa saa 48. Maafisa wa Hamas wamesema kuwa wanataka Haniyeh kuongoza baraza la mawaziri la serikali ya umoja wa kitaifa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW