1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH : Putin kuwasaidia Wapalestina

30 Aprili 2005

Rais Vladimir Putin wa Russia amekuwa na mazungumzo na kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas katika kituo cha mwisho cha ziara yake ya Mashariki ya Kati ambayo pia imemfikisha Israel na Misri.

Katika ziara yake ya kwanza kabisa katika Ukingo wa Magharibi Putin ameahidi kuimarisha mchakato wa amani na kuisaidia Mamlaka ya Palestina kulijenga upya jeshi lake la usalama.Russia imekuwa na shauku ya kutanuwa dhima yake katika jitihada za kutafuta amani Mashariki ya Kati. Mapema wiki hii Putin alipendekeza kuandaa mkutano wa amani katika kipindi cha majira pukutizi mwaka huu mjini Moscow.

Viongozi wa Palestina wamelikaribisha wazo hilo lakini limepuuzwa na Israel na Marekani kwamba ni mapema mno kuwa na mkutano huo.

Putin hivi sasa ameufuta mpango huo.