1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH. Putin Na Mahmud Abbas tayari wamefanya mkutano.

29 Aprili 2005

Kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas amefanya mazungumzo na rais Vladmir Putin wa Urusi katika ukingo wa magharibi na kumueleza kuwa wakati sasa umewadia kwa rais Putin kuongoza mashauri ya amani ya mashariki ya kati yaliyopangwa kufanyika mjini Moscow Urusi.

Rais Vladmir Putin ndio kiongozi wa kwanza wa Urusi kufika katika ukingo wa magharibi na hapo awali alikuwa amependekeza kwa nchi yake kuongoza mazungumzo ya amani ya mashariki ya kati lakini wazo hilo halikupokelewa vyema na Marekani na Israel na hivyo basi Urusi ikageuza nia yake juu ya jambo hilo mara tu rais Putin alipokutana na viongozi wa Israe katika ziara yake ya kihistoria ya mashariki ya kati.

Katika mkutano na waadnishi wa habari mjini Ramallah rais Putin ameiahidi Palestina msaada wa ndege za aina ya helicopter zitakazo saidia katika ujenzi mpya wa jeshi la Palestina.

Mapema katika ziara yake huko Israel rais Putin alipokea malalamiko juu ya Urusi kuiuzia Syria zana za kivita na kuiunga mkono Iran katika maswala ya Kinuklia.