1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH: Rais Abbas amevunja majadiliano na Hamas

17 Septemba 2006

Rais Mahmoud Abbas wa Wapalestina amevunja majadiliano ya kuunda serikali ya umoja kati ya chama chake Fatah na Hamas chenye siasa kali.Kwa mujibu wa msemaji wa Abbas,mazungumzo hayo yamevunjwa baada ya Hamas kusema kuwa hakitotambua makubaliano ya amani ya hivi sasa pamoja na Israel.Waziri mkuu Ismail Haniyeh wa chama cha Hamas lakini amekanusha ripoti hizo na akaeleza kuwa mazungumzo hayo yameahirishwa kwa sababu,wiki ijayo Rais Abbas atakuwepo Umoja wa Mataifa.Ni matumaini ya Wapalestina kuwa baada ya kuundwa serikali ya umoja wa Palestina,kati ya Hamas na chama cha wastani cha Fatah,vikwazo vya kimataifa vilivyowekwa tangu Hamas kushika madaraka miezi sita ya nyuma vitaondoshwa na misaada ya nchi za magharibi itarejea.Umoja wa nchi za Ulaya na Marekani zimeisusia serikali ya sasa inayoongozwa na Hamas kwa sababu inakataa kuitambua Israel na kusitisha kampeni ya kutumia nguvu dhidi ya taifa hilo la Kiyahudi.