1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ramallah: Rice azungumza na Wapalestina

18 Juni 2005

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani, Bibi Condoleezza Rice, amewasili kwenye makao makuu ya Utawala wa Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ambako atazungumza na Rais Mahmud Abbas. Amepokelewa na Waziri Mkuu, Ahmed Qorei, katika ofisi zake mjini Ramallah ambako Viongozi hawa wawili watazungumza. Mawaziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Masuala ya kiraia, Nasser al-Qidwa na Mohammed Dahlan nao pia watashiriki katika mazungumzo hayo. Bibi Rice amepangiwa kukutana na Rais Abbas leo jioni kabla ya kurejea mjini Jerusalem ambako atazungumza na Waziri Mkuu Ariel Sharon kesho Jumapili. Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani ameziomba Israeli na Palestina zishirikiane kwa dhati ili mpango wa Waisraeli wakutaka kuondoka katika Ukanda wa Gaza utekelezwe kikamilifu.