1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH : Sharon kukutana na Abbas tarehe 7 Juni

21 Mei 2005

Waziri Mkuu wa Israel Ariel Sharon na Rais Mahmoud Abbas wa Palestina wamepanga kukutana hapo tarehe 7 mwezi wa Juni .

Mkutano huo utakuwa wa pili kati yao na utafuatiwa na mazungumzo ya Abbas na Rais George W Bush wa Marekani yaliopangwa kufanyika Alhamisi mjini Washington.Kwa mujibu wa afisa mwandamizi wa Palestina Abbas na Sharon watakutana hapo Juni 7 baada ya viongozi huo kurudi kutoka Washington.

Maafisa wanasema viongozi hao watajadili njia za kudumisha usitishaji dhaifu wa mapigano waliokubaliana hapo tarehe 8 Februari katika mkutano wa amani wa viongozi uliofanyika nchini Misri.

Makubaliano hayo yamekuwa yakitishiwa na matukio kadhaa ya umwagaji damu katika siku za hivi karibuni katika Ukanda wa Gaza.