1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ramallah : Utawala wa ndani wa Palastina wasaka imani ya waisrael.

14 Machi 2005

Kiongozi wa utawala wa ndani wa Palastina Mahmoud Abbas amewasihi waisrael wauamini utawala wake.Akihojiwa na kituo cha televisheni cha Israel,rais Mahmoud Abbas amesema ufumbuzi wa mzozo kati ya Israel na Palastina utawezekana tuu kuputia mazungumzo ya amani.Rais Mahmoud Abbas ametetea umuhimu wa ujirani mwema pamoja na Israel.Ameurejea tena mwito wa kusitishwa ujenzi wa ukuta unaojengwa na Israel kuyazunguka maeneo ya ukingo wa magharibi.