1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH: Waziri Mkuu wa Israel AHMED QOREI ameitaka tena Israel ...

12 Januari 2004
isitishe ujenzi wa ukuta, kama isemavyo, kwa ajili ya usalama wake katika Ukingo wa Magharibi. Aliziomba Marekani, Ulaya, Urussi na Umoja wa Mataifa kuingilia kati, na akauelezea ukuta huo kama ni kipingamizi kikubwa katika mazungumzo yo yote ya kutafuta suluhisho la amani la Mashariki ya Kati. Na akaongeza ukuta huo ni mtengano wa kikabila. Israel inadai kizuizi hicho, ni muhimu ili kuwakinga Waisrael na magaidi wa kipalastina. Wapalastina wanasema ukuta huo ni kubakua ardhi zao.