1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ramallah: Waziri mkuu wa Palastina Ahmed Qorei amelaani hujuma ...

26 Desemba 2003

za madege ya kijeshi ya Israel katika Ggaza na shambulio la kusabilia maisha lililofanywa na wapalastina karibu na Telaviv.Amehimiza matumizi ya nguvu toka pande zote mbili yakome na kutetea haja ya kufikiwa haraka makubaliano ya kuweka chini silaha.Ahmed Qorei ametoa mwito wa kutiwa njiani haraka mpango mpya wa amani ulioandaliwa na Marekani,Umoja wa mataifa,Umoja wa Ulaya na Rashia.Msemaji wa waziri mkuu wa Israel Ariel Sharon amesema Israel haina budi isipokua kuchukua hatua kuulinda usalama wake.Hata hivyo msemaji wa waziri mkuu wa Israel amezungumzia umuhimu wa kuendelezwa mazungumzo ya daraja ya juu kati ya Israel na Palastina.Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Colin Powell,akihojiwa na kituo cha televisheni cha CNN,amemuonya waziri mkuu Sharon dhidi ya hatua za upande mmoja za kuufumbua ,atakavyo yeye ,mzozo wa mashariki ya kati.