1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH: Waziri Mkuu wa Palastina Ahmed Qorei ...

26 Desemba 2003
amelaumu vikali hujuma iliyolengwa makusudi na Israel mjini Gaza na pia shambulio la mpalastina la kuripua bomu kwa njia ya kujitolea mhanga. Alisema duru hizo za kulipizana kisasi lazima kusitishwa na pafikiwe muwafaka wa kuweka chini silaha baina ya pande mbili, - alielezea mkuu huyo wa serikali. Mpango wa amani wa pande zinazoitwa 4 unahitaji kutiwa vitendoni. Msemaji wa waziri mkuu wa Israel Ariel Sharon alitamka Israel inalazimika kuuhami usalama wake. Wakati huo huo, akasema, kuna haja ya kufanyika mazungumzo ya daraja za juu pamoja na wapalastina.