1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH

25 Mei 2005

Makamu waziri mkuu wa Palestina, Nabil Shaath, amesema wapalestina hawawezi kuandaa uchaguzi tarehe 17 mwezi Julai kufuatia tofauti zilizopo kati ya chama tawala cha Fatah na kundi la Hamas. Wabunge wa chama cha Fatah wametofautiana na rais Mahmoud Abbas juu ya mapendekezo yake ya kuzibadili sheria za uchaguzi.

Tangazo rasmi la kucheleweshwa kwa uchaguzi huo linatarajiwa kutangazwa na rais Abbas aliye ziarani nchini Marekani, ijapo amekuwa akisema kwamba uchaguzi huo utafanyika kama ilivyopangwa. Abbas atakutana na rais George W. Bush hapo kesho katika ikulu ya white house.