1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ramallah:Wateka nyara wataka waislamu waachiliwe katika magereza huko Marekani.

25 Agosti 2006

Hatua za tahadhari zinaendelea huko Ukingo wa Gaza kuwaokoa waandishi wa habari wawili waliokamatwa zaidi ya siku kumi sasa na wanamgambo.

Mateka hao wawli wanafanyia kazi katika kituo cha televisheni cha Marekani kijulikanacho kama Fox News, wameonekana katika matangazo ya video.

Watekaji nyara wao wanadai kuachiliwa huru kwa waislamu wanaoshikiliwa katika magereza nchini Marekani, lakini watu hao hawakusemi watawafanya nini mateka hao endapo hayakutekelezwa masharti yao.

Waziri Mkuu wa Palestina Ismail Haniya anaeongoza chama cha waislamu cha Hamas, ametoa mwito wa kuachiliwa huru kwa mateka hao bila ya kudhuriwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW