1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfrika Kusini

Ramaphosa anusurika kura ya kumuondoa madarakani

Hawa Bihoga
14 Desemba 2022

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ambae alikumbwa na kashfa, siku ya Jumanne alinusurika kura ya bungeni kuanzishiwa mchakato wa kumuondoa madarakani ambao ungeweza kumuondoa madarakani mapema kabla ya uchaguzi.

UK, London | Cyril Ramaphosa Präsident von Südafrika
Picha: Kirsty Wigglesworth/PA Wire/empics/picture alliance

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ambaye alikumbwa na kashfa siku ya Jumanne amenusurika katika kura iliyopigwa bungeni kuhusu iwapo ungeanzishwa mchakato ambao ungeweza kumuondoa madarakani mapema kabla ya uchaguzi.

Baada ya mjadala mkali chama chake cha African National Congress (ANC) kiliishinda hoja hiyo kwa kura 214 dhidi ya 148, huku watu wawili wakijizuia kupiga kura.

"Kwa hivyo uchunguzi hautaendelea" alisema spika wa Bunge la kitaifa la Afrika Kusini Nosiviwe Mapisa-Nqakula, akizuia kufunguliwa kwa mashitaka ya wizi wa kiwango kikubwa cha fedha katika shamba la Rais Ramaphosa.

Kuondolewa kwa Ramaphosa kungeliifanya nchi hiyo ilioendelea kiviwanda barani Afrika kutumbukia katika machafuko ya kisiasa.

Ramaphosa ambaye alitazamwa kama mwokozi katika masuala ya ufisadi baada ya mtangulizi wake kuchafuliwa kwa rushwa na ufisadi. Mtangulizi huyo, Jacob Zuma alipata pia uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa wabunge wa chama tawala ANC, ambacho nacho kinashuhudia mgawanyiko mkubwa kutokana na kashfa hiyo.

Soma pia: Kamati kuu ya ANC kuamua hatma ya Ramaphosa Afrika Kusini

Katika kikao cha bunge  kisichokuwa cha kawaida kilichoanza kwa kelele huko mjini Cape Town, ambacho kilijadili matokeo ya jopo huru ambalo lilisema Ramaphosa anaweza kuwa na hatia ya ukiukaji mkubwa na utovu wa nidhamu.

Rais Cyril Ramaphosa (katikati) akiondoka kwenye mkutano wa Kamati Kuu ya ANC mjini Johannesburg, Desemba 5, 2022, uliokuwa unajadili hatua za kuchukua kufuatia ripoti ya watalaamu iliyomtuhumu kuvunja kiapo chake cha urais.Picha: Jerome Delay/AP Photo/picture alliance

Rais huyo mwenye umri wa miaka 70,alinusurika kwenye sakata hilo kutokana na idadi kubwa ya wingi wa wabunge kutoka katika chama chake ANC.

Juma lililopita alipata uungwaji mkono tena  kutoka katika chama chake cha ANC katika bunge la kitaifa lenye idadi jumla ya viti 400 huku chama chake kikiwa na viti 230, baada ya kuwekwa kwa jaribio la kisheria lililotaka ripoti hiyo ifutiliwe mbali.

Hata hivyo baadhi ya wabunge wa chama chake hawakuwepo wakati wa zoezi la upigaji kura.

Waziri wa Sheria Ronald Lamola alipuuzilia mbali ripoti hiyo akisema "hakuna ushahidi wa kutosha kumshtaki rais".

ANC yaapa kutupilia mbali jaribio la kumuondoa Ramaphosa

Mtendaji mkuu wa ANC aliapa wiki iliopita kuwa watatupilia mbali jaribio lolote la kumlazimisha Ramaphosa kuondoka madarakani.

Baadhi ya watu walionekana kusikitishwa na uwamuzi huo na kusema kwamba huenda mtendaji huyo alikuwa na mkono wake kwa katika maamuzi ya wabunge.

Wabunge wachache wa ANC, akiwemo Nkosazana Dlamini-Zuma ambaye ni  mpinzani wa Ramaphosa, waziri wa baraza la mawaziri na mke wa zamani wa Zuma,  walikaidi amri ya chama.

Soma pia: Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa asema atautetea wadhfa wake kisasa na kisheria

Mtangulizi wa Ramaphosa aliyechafuliwa na ufisadi, Zuma alinusurika kwa hoja kadhaa za kutokuwa na imani naye wakati wa uongozi wake kabla ya chama chake kumlazimisha kujiuzulu mnamo 2018.

Hata hivyo vyama vya upinzani vilichukua msimamo mmoja kuhusiana na sakata hiloo.

Julias Malema ambae ni kiongozi na mwanasiamsa mwenye misimamo mikali kutoka chama cha pili kwa ukubwa cha upinzani cha Economic Freedom Fighters, alionyesha "kusikitishwa zaidi" na Ramaphosa ambaye ni mmoja wa watungaji wa katiba ya Afrika kusini.

Alisema Ramaphosa sasa ni mhalifu wa katiba ambaye "anakanyaga"  waraka huo, akimwita "mkiukaji wa katiba".

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma akiingia chumba cha mahakama mjini Pietermaritzburg, Afrika Kusini, Januari 31, 2022. Zuma aliondolewa madarakani kwa tuhuma za rushwa. Picha: Jerome Delay/Pool via REUTERS

Vuyolwethu Zungula, kiongozi wa African Transformation Movement, chama kidogo cha upinzani ambacho kiliwasilisha hoja ya uchunguzi ulioidhinishwa na bunge kuhusu kashfa hiyo, alisema "wakati utathibitisha kwamba hakuna mtu aliye juu ya sheria".

Ramaphosa, ambaye alikuwa nyumbani kwake wakati wa upigaji kura, alianza siku yake katika mji mkuu wa Pretoria, akihudhuria sherehe ya kuhitimu kwa mafunzo ya  maafisa wa jeshi la polisi.

Iwapo upinzani ungekuwa na njia yake, Ramaphosa angekabiliwa na uwezekano wa suala hilo kuchunguzwa zaidi na bunge katika mwaka mmoja kuelekea uchaguzi mkuu wa 2024.

Kura ya kumuondoa madarakani ingelihitaji kuungwa mkono na theluthi mbili ya wabunge.

Mzizi wa shutuma za Ramaphosa

Rais, ambaye alikuwa mfanyabiashara tajiri kabla ya kujitosa rasmi kwenye ulingo wa siasa, alijikuta kwenyewakati mgumu mwezi Juni, wakati mkuu wa zamani wa kitengo cha ujasusi mwenye utata alipowasilisha malalamiko dhidi yake kwa jeshi la  polisi.

Soma pia: Hatima ya kisiasa wa rais Ramaphosa iko matatani

Arthur Fraser alidai Ramaphosa alificha wizi wa dola milioni kadhaa kutoka kwa shamba lake mnamo 2020.Alimshutumu rais kwa kuwateka nyara wezi hao na kuhongwa kimya badala ya kuripoti suala hilo kwa mamlaka.

Rais mpya wa Afrika Kusini, Ramaphosa

01:03

This browser does not support the video element.

Ramaphosa hajashtakiwa kwa uhalifu wowote na amekana kutenda makosa.  Matokeo ya uchunguzi huo maalum wa watu watatu, uliotolewa wiki iliyopita, ulileta maelezo ambayo yameondoka Afrika Kusini.

Ramaphosa alikiri wizi wa dola 580,000 za pesa taslimu ambazo zilifichwa chini ya sofa kwenye shamba lake, mahali ambapo wafanyakazi wake walisema ni salama kuliko kwenye sefu ya ofisi yake.

Alisema fedha hizo ni malipo ya nyati walionunuliwa na mfanyabiashara wa Sudan, ambaye hivi karibuni alithibitisha shughuli hiyo katika mahojiano na vyombo vya habari vya Uingereza.

Chanzo: AFPE

     

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW