1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ramaphosa asema bunge Afrika Kusini kufunguliwa Julai 18

28 Juni 2024

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema leo kuwa bunge litafunguliwa kwa muhula wake ujao mnamo Julai 18 katika wakati ambapo anaendelea na mazungumzo na vyama vyengine kuunda baraza la mawaziri.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa Picha: Kim Ludbrook/Pool/EPA

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema leo kuwa bunge litafunguliwa kwa muhula wake ujao mnamo Julai 18 katika wakati ambapo anaendelea na mazungumzo na vyama vyengine kuunda baraza la mawaziri licha ya kuweko kwa ripoti za mzozo kati ya vyama vinayounda serikali.

Mazungumzo juu ya kuteua baraza la mawaziri yamekuwa yakiendelea kwa wiki mbili sasa japo yamegubikwa na tofauti kati ya chama cha Ramaphosa cha ANC na kile cha Democratic Alliance DA, chama cha pili kwa ukubwa nchini humo, kuhusu jinsi ya kugawanya nyadhifa za mawaziri. Soma: ANC: Makubaliano ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa yamepatikana

Mazungumzo kati ya vyama hivyo viwili yaliovujishwa yameonyesha kuwepo kwa mvutano.

Katika mojawapo ya barua ambazo Ramaphosa amemuandikia kiongozi wa chama cha DA John Steenhuisen, rais huyo amekishtumu chama cha DA kwa kubadili msimamo na kutaka nyongeza ya idadi ya nafasi za uwaziri kutoka sita hadi nane, na hivyo basi kuhatarisha makubaliano ya muungano huo mpya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW