1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ramaphosa kuapishwa kwa muhula mwengine Afrika Kusini

19 Juni 2024

Rais mteule wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, anatarajiwa kuapishwa ili kuanza muhula mpya kama rais katika hafla itakayofanyika mjini Pretoria leo Jumatano.

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini.
Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini.Picha: Nic Bothma/REUTERS

Hatua hiyo ni baada ya chama chake cha African National Congress (ANC) kufikia makubaliano ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Wabunge walipiga kura kwa wingi kumchagua tena Ramaphosa mwenye umri wa miaka 71 wiki iliyopita, baada ya kumalizika uchaguzi mkuu wa Mei 29, ambao haukutowa mshindi wa moja kwa moja.

Soma zaidi: Biden ampongeza Ramaphosa kuchaguliwa tena Afrika Kusini

Ramaphosa ataapishwa kuhudumu muhula mpya wa miaka mitano katika hafla itakayohudhuriwa na wabunge, viongozi wa kigeni, viongozi wa kidini na kimila na wageni wengine katika majengo ya makao makuu ya serikali.

Ofisi ya rais imesema takribani wakuu wa nchi 18 za Afrika watahudhuria hafla hiyo.

China, Misri, Cuba, Zimbabwe na Mamlaka ya Palestina ni miongoni mwa nchi zitakazowakilishwa na maafisa wa ngazi za juu, imesema ofisi ya rais.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW