1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfrika Kusini

Ramaphosa kulihutubia taifa huku kukiwa na uhaba wa umeme

9 Februari 2023

Rais wa Afrika Kusini ambaye hivi leo anatarajiwa kulihutubia taifa, anakabiliwa na shinikizo la kuwashawishi raia kuwa serikali yake inashughulikia vyema tatizo kubwa la uhaba wa umeme na hali mbaya ya kiuchumi.

Südafrikas Präsident Cyril Ramaphosa
Picha: Themba Hadebe/AP/dpa/picture alliance

Ramaphosa atafungua kikao kipya cha Bunge mjini Cape Town wakati Afrika Kusini, yenye uchumi mkubwa zaidi barani Afrika, ikikabiliwa na matatizo ya kukatika kwa umeme kwa muda mrefu, viwango vya juu vya ukosefu wa ajira, mfumuko wa bei za vyakula na mafuta.

Afrika Kusini imeshuhudia pia maandamano makubwa ya jamii za watu maskini wanaoitupia lawama serikali kwa kushindwa kutoa huduma muhimu kama vile maji safi na makaazi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW