RANGOO:Maandamano yaendelea kuupinga utawala wa kijeshi nchini Burma
24 Septemba 2007Matangazo
Nchini Burma zaidi ya watu elfu 10 wakiongozwa na watawa wa dini ya kiBudda wameandamana katika mji mkuu Rangoo kupinga utawala wa kijeshi nchini humo.
Zaidi ya watawa wa kike 150 wa dini hiyo ya kibudda walijiunga katika maandamano hayo.
Hiyo ni siku moja tu baada ya watawa hao kukutana na kiongozi wa upinzani Aung San Suu Kyi ambaye alikuwa katika kifungo cha nyumbani kwake toka mwaka 2003.
Viongozi wa maandamano hayo wameahidi kuendelea kuandamana hadi pale utawala wa kijeshi wa nchi hiyo utakapoanguka.
Upinzani ulianza mwezi uliyopita baada ya serikali kupandisha mara mbili bei ya mafuta.