RANGOON: Gambari kukutana na Aung San Suu Kyi
6 Novemba 2007Matangazo
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa,Ibrahim Gambari akifanya ziara yake ya pili nchini Burma, amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje,Nyan Win na viongozi wa makundi ya kikabila katika juhudi ya kuihimiza utawala wa kijeshi kufanya mageuzi nchini humo.Gambari anatazamia pia kukutana na kiongozi wa upinzani anaegombea demokrasia,Aung San Suu Kyi aliewekwa katika kizuizi cha nyumbani.Kwa mujibu wa serikali ya Burma,Gambari hatokutana na Jemadari Mkuu Than Shwe.
Kwa upande mwingine watawa wa Kibudha kwa mara nyingine tena,wamefanya maandamano ya amani kuunga mkono demokrasia.Mnamo mwezi wa Septemba utawala wa kijeshi ulitumia nguvu kuzuia maandamano makubwa.Watu 13 waliuawa na maelfu wengine wametiwa ndani.