1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RANGOON: Waandamanaji wafyatuliwa risasi Burma

28 Septemba 2007

Licha ya kushinikizwa na jumuiya ya kimataifa, serikali ya kijeshi nchini Burma,imeendelea kuchukua hatua kali dhidi ya waandamanaji katika mji mkuu Rangoon.

Vikosi vya usalama vimefyatulia risasi watawa na raia wa kawaida waliokuwa wakiandamana kupinga utawala wa kijeshi.Vyombo vya habari vimesema,watu 9 wameuawa,akiwemo mwandishi wa habari wa Japani.Vile vile kiasi ya watu 40 wamejeruhiwa.