1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Rasi mpya wa Taiwan aapa kuilinda demokrasia ya kisiwa hicho

20 Mei 2024

Rais mpya wa Taiwan Lai Ching-te ameapa kuilinda demokrasia ya kisiwa hicho huku akiitolea mwito China kusitisha uchokozi wake wa kijeshi dhidi ya kisiwa hicho kinachojitawala chenyewe.

Taiwan, Taipei | Rais mpya wa Taiwan Lai Ching-te akiwapungia mkono raia katika sherehe za kuapishwa kwake.
Rais mpya wa Taiwan Lai Ching-te akiwapungia mkono raia katika sherehe za kuapishwa kwake.Picha: Sam Yeh/AFP/Getty Images

Rais Lai amesema "nataka kuitolea mwito China kuachana na kitisho chake cha kijeshi na kisiasa dhidi ya Taiwan na  kuwa na Jukumu la Kimatifa la kudumisha amani na uthabiti katika ujia wa Bahari wa Taiwan na kuhakikisha dunia ipo huru kutokana na hofu ya vita." 

Beijing ambayo awali ilimuelezea Lai kama mtu hatari ilijibu kwa kutoutambua Uhuru wa Taiwan. 

Soma pia:Lai Ching-te aapishwa rasmi kuwa rais mpya wa Taiwan

Katika hotuba yake aliyoitoa baada ya kuapishwa, Lai alizungumzia moja kwa moja kitisho cha vita kufuatia miaka mingi ya juhudi za China kutaka kuidhibiti Taiwan, akisema demokrasia ya kisiwa hicho imeimarika na kuwashukuru raia kukataa kuyumbishwa na nguvu za nje na kwa kuitetea demokrasia hiyo.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW