Ratiba ya msimu mpya wa EPL yatangazwa
17 Juni 2015Matangazo
Manchester City iliomaliza katika nafasi ya pili pointi nane nyuma ya Chelsea itaelekea West Bromwich huku Manchester United ikikabiliana na Tottenham katika uwanja wa Old Trafford.
Arsenal itaialika West Ham, Liverpool itaenda Stoke katika mchuano unatarajiwa kuwa mgumu, Newcastle itakabiliana na Southampton huku Leicester ikiialika Sunderland nyumbani.
Bournemouth iliopandishwa daraja msimu huu, Watford na Norwich zitakabiliana na Aston Villa, Everton na Crystal Palace mtawalia.
Msimu huu wa 2015/2016 utanza wiki moja mapema ikilinganishwa na msimu uliopita
Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Mohamed Khelef