Rau nchini Tanzania
20 Machi 2004Matangazo
ARUSHA: Rais wa Ujerumani Johannes Rau akiwa ziarani Tanzania, hii leo atakutana na Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ya Rwanda, Erik Mose. Mahakama hiyo iliyoundwa na UM huko Arusha, Tanzania ya Kaskazini, imekabidhiwa jukumu la kuchunguzi mauwaji ya halaiki yaliyofanyika nchini Rwanda ambamo inasemekana mwaka 1994 waliuawa Watusi na Wahutu wapatao 800,000. Baada ya Nigeria Tanzania ni nchi ya pili kutembelewa na Rais Johannes Rau wa Ujerumani na Mkewe Christina katika ziara yao ya nchi za Kiafrika.
