1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoRwanda

Rayon Sport yashindwa ligi kuu Rwanda

19 Desemba 2022

Huku ikisalia mechi moja ya ligi kuu ya soka daraja la kwanza nchini Rwanda, AS Kigali wanaongoza ligi. APR FC imeichapa Rayon sports bao 1-0 katika uga wa Kigali Nyamirambo.

Adidas Finale Istanbul 21 Ball
Picha: Laszlo Balogh/AP Photo/picture alliance

Ilikuwa huzuni na majonzi makubwa kwa wachezaji, wapenzi,mashabiki na viongozi wa Rayon Sports kushindwa  kuifunga kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo na APR FC kufuatia kichapo cha bao1-0 katika uwanja wa Kigali Nyamirambo.

Kocha mkuu wa Rayon Francis Haringingo alisema "Mambo yakienda kombo  watu wanaona mengi, lakini mchezo katika kipindi cha kwanza tumecheza vizuri  na tumepata nafasi za kufunga lakini haikuwzekana.Katika kipindi cha pili wao pia wamekuja wakiwa imara , tumefanya kosa wakatufunga bao lakini ndo hivo mchezo tulikuwa tumeandaa  vizuri."

Bizimana Yannick ambaye alisajiliwa na Apr miaka miwili iyopita kutoka club ya Rayon, kunako dakika ya 74 aliwaamsha mashabiki wa timu ya jeshi la Rwanda APR  ambapo alipokea pasi safi kutoka kwa Ishimwe Anicet na kuweka kimyani bao la pekee.

Timu ya Misri yatamba

Tukiangazia  fainali ya vilabu bingwa barani Afrika mpira wa kikapu wanawake, timu ya Alexandria Sporting ya Misri imetawazwa mabingwa  baada ya kufunga  Costa de sol ya Angola kwa alama 65- 58 mjini Maputo, Msumbiji.

Kuania nafasi ya 6 na 7,  Mwakilishi wa Rwanda katika kombe hilo la vilabu bingwa APR Basketball, ambayo imetulia katika nafasi 7 baada ya kuzabwa na  CNSS kutoka  DRC kwa alama 72-52.

Na Timu ya Bandari ya Kenya KPA imeshikilia nafasi ya 6 katika mashindano ya fainali ya kombe la Afrika.

Hii ni mara ya kwanza APR kushiriki fainali za kombe la Afrika wanawake.

 

//Christopher Karenzi

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW