Real Madrid hoi bin taaban kwa Barcelona
30 Novemba 2010Matangazo
Kufuatia ushindi huo mkubwa ambao haukutarajiwa, Barcelona sasa wako kileleni mwa ligi hiyo kwa pointi mbili zaidi ya mahasimu wao hao.
Barcelona waliwaburudisha vilivyo washabiki waliyofurika katika uwanja wao wa Nou Camp kwa kandanda safi, lililowafanya Real Madrid timu iliyosheheni wachezaji nyota, kuhangaika kutafuta mpira muda mwingi wa mchezo.
Mabao ya Barcelona yaliwekwa wavuni na Xavi,Pedro na David Villa, ambaye mara baada ya mchezo alisema walikuwa bora zaidi dimbani kuliko wapinzani wao.
Real inayofundishwa na Jose Morinho ilishuhudia beki wake Sergio Ramos akipewa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya Lionel Messi.
Mwandishi:Aboubakary Liongo
Mhariri:Othman Miraji