1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Madrid washinda taji la 14 la Ligi ya Mabingwa

29 Mei 2022

Real Madrid wameishinda Liverpool na kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya

Champions-League-Finale - Liverpool vs. Real Madrid
Picha: Lee Smith/REUTERS

Bao moja la Vinicius Junior kunako dakika ya 59 lilitosha kuihakikishia Real ushindi wa 14 wa kombe la Ulaya mbele ya mashabiki 80,000 mjini Paris.

Real Madrid kwa mara nyingine inarejea nyumbani na kombe, Madrid imetumia fursa na kuwaacha wengi wakijiuliza ni kwa jisi gani wameambulia ushindi wa konbe hilo. 

soma Liverpool yatinga fainali ya ligi ya mabingwa

Jaribio la mshambuliaji Karim Benzema liliamuliwa kwa utata kuwa ameotea.

Mchezaji wa Liverpool Mohamed Salah akinyimwa nafasi ya kuikomboa mara tatu timu yake na mlinsa lango wa Real Madrid Thibaut Courtois.

Usalama uwanjani

Picha: Petr David Josek/AP/picture alliance

Fainali hio ilicheleweshwa kwa zaidi ya dakika 35 kwa sababu za usalama.

Shirikisho la Kandanda Barani Ulaya UEFA ililaumu kuchelewa kuwasili kwa mashabiki, lakini mashabiki walilaumu mamlaka kwa kuchelewa kufungua uwanja wa Stade de France.

Mamia ya mashabiki wa Liverpool walimiminika kujaza viti katika uwanja wa Stade de France, polisi wa Ufaransa walilazimika kutumia gesi ya kutoa machozi ili kuwazuia.

"Tumesikitishwa sana na maswala ya kuingia uwanjani na uharibifu wa eneo la usalama ambalo mashabiki wa Liverpool walikabiliana nao jioni ya leo huko Stade de France," ilisoma taarifa iliyotolewa na Liverpool katika kipindi cha pili.

"Hii ni mechi kubwa zaidi katika soka la Ulaya na wafuasi hawapaswi kuwa na matukio ambayo tumeshuhudia usiku wa leo. Tumeomba uchunguzi rasmi kuhusu sababu za masuala haya yasiyokubalika."

soma pia Ancelotti: Madrid iko sawa kuonekana wanyonge dhidi ya Manchester City

Ngoma itambae

Picha: Jonathan Nackstrand/AFP/Getty Images

Mlinda lango wa Madrid Courtois alikuwa muhimu, na kuokoa kombora kutoka kwa Mo Salah na kumfanya mchezaji bora wa mechi. Lakini kwa uzoefu, na mfululizo wa kujimbanua ilikuwa uchawi tosha kwa timu ya Real Madrid.

 

 https://p.dw.com/p/4BzW3

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW