1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Regragui atarajia ushindi nusu fainali ya AFCON

14 Januari 2026

Kocha wa Morocco, Walid Regragui anatarajia ushindi katika nusu fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika huku timu nne bora za bara hilo na zenye uwezo wa kushinda taji hilo zikitarajiwa kuingia dimbani Jumatano usiku.

Kombe la Mataifa ya Afrika 2025 | Mechi ya hatua ya makundi | Morocco dhidi ya Mali | Timu ya taifa ya Morocco
Timu ya Morocco wakati wa mechi ya Kundi A la AFCON kati ya Morocco na Mali katika Uwanja wa Complexe Sportif Prince Moulay Abdellah, Rabat, Morocco mnamo Desemba 26, 2025.Picha: Bouhara Hamza/abaca/picture alliance

Morocco itakutana na Nigeria katika nusu fainali ya pili baada ya Senegal kukabiliana na mabingwa mara saba wa AFCON, Morocco. Waliwahi kukutana kwenye fainali za mwaka 2021, na Senegal ikaibuka mshindi.

Regragui amesifia si tu ubora wa viwanja bali pia hali nzuri ya hewa na wachezaji bora ulimwenguni katika nusu fainali hii ikiwa ni pamoja na Mo Salah, Ashraf Hakimi, Ademola Lookman na Sadio Mané na kuongeza kuwa hii inatoa nafasi ya kuonyesha ubora wa bara la Afrika kwenye soka la ulimwengu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW