1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
KandandaUlaya

England waiadhibu Uhispania nyumbani

16 Novemba 2026

Nahodha wa England Harry Kane anasema ushindi wa England dhidi ya Uhispania ni mkubwa mno na unaonesha jinsi mchezo wao ulivyoimarika.

Ligi ya Ulaya UEFA 2018 | Uhispania vs. England | Harry Kane akicheza
Nahodha wa England Harry Kane Picha: Miguel Morenatti/AP Photo/picture alliance

Kane anasema mchezo wao umerimarika tangu mashindano ya Kombe la Dunia, kiasi cha hata timu bora duniani kutoweza kuwafunga.

Mwaka uliokuwa na hekaheka nyingi uliishia kimtindo siku ya Jumapili mjini Madrid, baada ya mabingwa wa dunia na Ulaya kulazwa na vijana wa Thomas Tuchel waliokuwa na hamu sana ya ushindi.

Harry Kane aliwatia England uongozini kwenye kipindi cha kwnaza halafu Ezri Konsa na Ben White wakaongeza mabao mengine mawili na kuwapelekea England kuwa kifua mbele 3-0.

Hakuna mechi nzuri ya kuonyesha ubora mechi kama dhidi ya Uhispania

Mabadiliko ya Uhispania yaliwapelekea kupatamabao mawili kupitia kwa Mikel Oyarzabal aliyefunga mkwaju wa penalti baada ya Elliot Anderson kuoneshwa kadi nyekundu halafu Nico Williams akaongeza la pili la Uhispania ila England walijilinda vyema na kuhakikisha wanaivunja rekodi ya mechi 43 ya kutofungwa ya La Furia Roja.

Nyota wa Uhispania Lamine YamalPicha: Tom Weller/dpa/picture alliance

"Kabla mashindano ya Ligi ya Ulaya tulizungumza kwamba tunataka kutumia mechi hizi kuimarika kwa kweli, kuonesha utambulisho wetu na jinsi tunavyotaka kusonga mbele katika siku zijazo," alisema nahodha Harry Kane. "Na hakuna mechi nzuri zaidi ya kuonesha uwezo wetu kama dhidi ya Uhispania ugenini baada ya kwenda zaidi ya mechi 40 bila kufungwa. Kabla kadi nyekundu, tulikuwa tumewalemea, tulikuwa makini na hawakuweza kudhibiti shinikizo."

Kane anasema mchezo huo wa kuwavamia wapinzani walionesha jana ambao Uhispania haikuweza kuudhibiti, unastahili kuwapa imani.

Kwengineko Ufaransa walipata ushindi wa 2-1 walipocheza na Uturuki huku timu waliyo nayo kwenye kundi moja Ubelgiji, ikiilemea Italia 4-1 katika mechi nyengine iliyochezwa Jumapili.

Ufaransa waliingia kwenye mechi hiyo baada ya kupondwa pondwa na Italia 3-1 mnamo siku ya Ijumaa.

Ufaransa sasa imefuzu kwenye robo fainali ya mashindano hayo ya Ligi ya Ulaya pamoja na Ubelgiji ila Italia imekosa nafasi ya kusonga mbele.

Imehaririwa na:Bruce Amani
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW