Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani aondolewa
4 Oktoba 2023Tukio hilo linafichua viwango vya ndani vya machafuko kati ya Warepublican wanaoelekea kwenye uchaguzi wa urais wa 2024, na bila shaka ukioongozwa na Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, ambaye anaweka historia yake kama rais wa kwanza wa zamani anaelengwa kuwa na mashtaka mengi ya jinai.
Wabunge 8 wa chama cha Republican Matt Gaetz, Tim Burchett, Andy Biggs, Ken Buck , Matt Rosendale, Eli Crane, Bob Good na Nancy Mace walipiga kura kwa kushirikiana na wabunge wote wa upande wa chama cha Demokrat kumwondoa McCarthy, ambaye kwa sasa anasalia kuwa mbunge wa kawaida baada ya kuondoka katika kiti cha uspika.
Tukio la kwanza kihistoria kwa miaka 234.
Hilo linakuwa tukio la kwanza la kuondolewa kwa spika katika historia ya miaka 234 ya Bunge liliungwa mkono na wafuasi wachache wa chama cha Republican wenye misimamo mikali ya mrengo wa kulia.
McCarthy anakuwa kuwa spika wa kwanza katika historia ya Marekani kuondolea kwa 269 , kufuatia uasi kati ya wabunge wa siasa kali za mrengo wa kulia ambao wanahudumu ikiwa ni ishara ya wazi ya kugawanyika Chama cha Republican.
Mfanyabiashara wa zamani mwenye umri wa miaka 58 ambaye kwa wakati huo alipokuwa akitoka nje ya ukumbi hakusema lolote, alizua ghadhabu miongoni mwa wahafidhina alipopitisha hatua ya ufadhili ya mwishoni mwa juma iliyoungwa mkono na Ikulu ya Marekani White House ili kuepusha kufungwa kwa shughuli za serikali.
Kiini cha kuondolewa Kevin McCarthy
Kiini cha hatua hiyo ni Mbunge Matt Gaetz ambae Jioni ya Jumatatu alianzisha hoja ya kumuondoa spika huyo kwa kushirikiana na Wademokrat kupitisha mpango wa matumizi kwa siku 45 ili kuzuia kufungwa kwa shughuli za serikali.
Baada ya tukio hilo Matt Gaetz alisema sababu za kuondolewa kwa kiongozi huyo ni kwamba hakuna anaemuamini kwa kuwa amekuwa akitoa ahadi nyingi zinazokinzana. Nafasi yake kwa sasa inazibwa kwa muda na Mbunge Patrick McHenry wa Republican, hilo ni kwa mujibu wa kanuni za bunge ambazo zilimtaka McCarthy kutoa orodha ya watakaochukua nafasi za muda iwapo nafasi itakuwa wazi.
Soma zaidi:Marekani kutumbukia katika mzozo wa kiuchumi
McHenry, mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Kifedha ya Baraza la Wawakilishi, ni mshirika wa McCarthy pia na alizungumza kumuunga mkono kabla ya kura.
Vyanzo: AFP/DW