Riek Machar kufanya ziara nchini Sudan Kusini
9 Septemba 2019Kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini anayeishi uhamishoni, Riek Machar anatarajiwa kufanya ziara yake ya kwanza baada ya mwaka mmoja mjini Juba leo Jumatatu.
Machar atafanya mazungumzo na Rais Salva Kiir, hayo ni kwa mujibu wa vyanzo kutoka serikalini na upande wa upinzani vilivyozungumza na shirika la habari la AFP.
Msemaji wa serikali ya Sudan Kusini Michael Makuei viongozi hao wanatarajiwa kujadili masuala muhimu kuhusiana na makubaliano ya amani na pia namna ya kusonga mbele.
Mwanachama mmoja wa ngazi ya juu katika chama cha SPLM-IO Kang Pal Chol, amesema ziara ya bwana Machar, nchini Sudan Kusini ni dhmaira ya amani.
Mkutano huo unafanyika huku tarehe ya mwisho ya kuunda serikali ya kugawana madaraka. Baada ya Rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek machar kutia saini makubaliano ya amani mnamo mwaka 2018 kumekuwa na migogoro mingi ambayo imesabisha kuchelewa kuundwa kwa serikali hiyo ya maridhino ya kugawana madaraka.