1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rigathi Gachagua asema ulinzi wake umeondolewa

21 Oktoba 2024

Makamu wa rais wa Kenya aliyeondolewa, Rigathi Gachagua, amesema kikosi chake cha ulinzi kimeondolewa na hivyo basi Rais William Ruto atawajibika iwapo lolote litamtokea.

Makamu wa rais wa Kenya aliyeondolewa, Rigathi Gachag
Makamu wa rais wa Kenya aliyeondolewa, Rigathi GachaguaPicha: Andrew Kasuku/AP/picture alliance

Makamu wa rais wa Kenya aliyeondolewa, Rigathi Gachagua, amesema kikosi chake cha ulinzi kimeondolewa na hivyo basi Rais William Ruto atawajibika iwapo lolote litamtokea.

Gachagua, ambaye anapinga mashtaka dhidi yake akisema yamechochewa kisiasa, amewaambia waandishi wa habari kwamba usalama wake uko hatarini.

Msemaji wa polisi Bi. Resila Onyango, alikataa kutoa maoni yake mara moja na amesema atafanya uchunguzi kuhusu kauli ya Gachagua kuhusu ulinzi wa usalama wa kiongozi huyo. Msemaji wa Rais Ruto amewaambia waandishi wa habari kwamba watatoa maoni yao baadaye.Gachagua atimuliwa wakati akiugua hospitali

Ulinzi wa hali ya juu hupunguzwa kwa wanasiasa wakuu baada ya kuondoka madarakani nchini Kenya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW