1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripoti: HRW yailaumu Tanzania kwa kuikuka haki za Wamaasai

31 Julai 2024

Shirika la kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch katika ripoti yake ya tarehe 31.07.2024, limesemaTanzania inawafurusha kwa nguvu maelfu ya watu wa jamii ya Wamaasai kutoka kwenye ardhi ya mababu zao.

Tanzania Arusha | Wamaasai kwenye hifadhi ya Ngorongoro
Tanzania Arusha | Wamaasai kwenye hifadhi ya NgorongoroPicha: Huax Hongli/Xinhua/IMAGO

Shirika la Human Rights Watchkwenye ripoti yake hiyo limebainisha matukio ya kikosi cha askari wanaosimamia hifadhi za wanyamapori wakiwashambulia na kuwapiga wakazi katika eneo hilo huku kukiwa hakuna adhabu yoyote inayochukuliwa dhidi ya maafisa hao.

Ripoti hiyo pia imesema wanajamii 13 wametoa madai ya kupigwa kati ya Septemba 2022 na Julai 2023.

Makaazi ya jamii ya Wamaasai katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro, Arusha TanzaniaPicha: Huax Hongli/Xinhua/IMAGO

Walinzi hao wa hifadhi za wanyamapori nchini Tanzania ni kama watu walio juu ya sheria imesema ripoti hiyo ambayo pia imedai kuwa serikali ya Tanzania haikuwapa watu wa jamii ya Wamaasai haki ya kujiamulia iwapo wanaridhia kuhamishwa hali ambayoHRW imesema inakiuka haki za kumiliki ardhi, kupata elimu na huduma za afya kwa wanajamii wanaohamishwa kwa nguvu.

Soma Pia: Hatua ya Tanzania kuwaondoa Wamasai yazidi kuibua hisia 

Human Rights Watch imesema mvutano wa muda mrefu kati ya serikali ya Tanzania na jamii ya wafugaji ya Wamaasai wakati mwingine umesababisha vurugu mbaya, tangu serikali ilipoanzisha mpango wa kuihamisha jamii hiyo kuanzia mwaka 2022. 

Takriban watu 82,000 wanatakiwa kuhamishwa kutoka eneo maarufu duniani la Hifadhi ya Ngorongoro na kupelekwa katika wilaya ya Handeni, iliyo umbali wa takriban kilomita 600 kutoka kwenye eneo lao hadi ifikapo 2027.

HRW imesema iliwahoji karibu watu 100 kati ya Agosti 2022 na Desemba 2023, wakiwemo wanajamii ambao tayari wameshahamia kwenye kijiji cha Msomera huko Handeni na wengine ambao bado wanakabiliwa na hali hiyo ya kuhamishwa.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu HassanPicha: Daniel Pier/NurPhoto/picture alliance

Ripoti hiyo imesema ili kuwashinikiza watu wa eneo hilo kukubali kuondoka mamlaka ilizuia upatikanaji wa huduma muhimu kwa kupunguza ufadhili katika ujenzi wa miundombinu ya shule vituo vya afya na hivyo watu hao inawalazimu kwenda mwendo mrefu ili kupata huduma hizo.

Soma Pia: Serikali ya Tanzania imesema hakuna mapambano yoyote kati ya askari polisi na wananchi

Serikali ya Tanzania imesema hatua yake ni kwa ajili ya kulihifadhi eneo hilo dhidi ya uvamizi wa binadamu kutokana na kwamba eneo hilo ni Turathi ya Dunia lililoorodheshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa, UNESCO. Lakini HRW imesema serikali ya Tanzania itaitumia ardhi hiyo kwa madhumuni ya kukuza utalii.

Hatua hiyo ya serikali ya Tanzania imekosolewa kimataifa huku Benki ya Dunia na Umoja wa Ulaya zikisimamisha ufadhili wa fedha. Benki ya Dunia ilisitisha malipo ya dola milioni 150 mnamo mwezi Aprili fedha ambazo zingelitumiwa kuhifadhi mbuga na Umoja wa Ulaya pia umebatilisha ustahiki wa Tanzania wa kupokea ufadhili wa dola milioni 19 kwa ajili hiyohiyo ya kuhifadhi mbuga.

Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Human Rights Watch (HRW) Kanda ya Afrika, Laetitia BaderPicha: Human Rights Watch

HRW imesema imegundua kwamba serikali inawanyamazisha wakosoaji hali inayochangia pakubwa watu kuwa na hofu. Imemnukuu mtu mmoja ambaye tayari ameshahamia katika kijiji kipya cha Msomera akisema  "Mtu hawezi kusema lolote.”

Chanzo:AFP

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW