1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Ripoti: Jeshi la Israel lilitahadharishwa kabla ya Oktoba 7

18 Juni 2024

Ripoti zasema Jeshi la Israel lilitahadharishwa juu ya shambulizi la Oktoba 7, wiki mbili kabla.

Israel Süd-Israel | Israelische Soldaten
Picha: Jim Hollander/UPI Photo/Newscom/picture alliance

Shirika la Utangazaji la Umma nchini Israel, Kan limeripoti hii Jumanne kwamba Idara ya Ujasusi ya Israel ilitahadharisha juu ya shambulizi linalotarajiwa kufanyika wiki mbili kabla Hamas hawajaishambulia Israel Oktoba 7, kutokea Ukanda wa Gaza.

Ripoti ya Kan imesema mipango ya kushambulia kambi za kijeshi na makaazi na kwachukua mateka 250 ilipangwa kwenye waraka uliosambazwa ndani ya Kitengo cha Gaza cha Jeshi la Ulinzi la Israel, IDF, Septemba 19.

Ripoti hiyo ya hadhari ilitolewa na kitengo cha IDF kinachohusika na kukusanya taarifa za kijasusi cha 8200 lakini hata hivyo ilipuuzwa na maafisa waandamizi.

Na kilichozingatiwa kama kitisho zaidi kilikuwa ni mpango wa magaidi waliopanga kuingia Israel kupitia vituo vitatu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW