1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripoti: Jeshi la Sudan lilitumia silaha za kemikali

9 Oktoba 2025

Ripoti za vyombo vya habari zilizotolewa leo, zinaonyesha kuwa jeshi la Sudan lilitumia gesi ya klorini katika mashambulizi mawili mwaka 2024, kaskazini mwa mji mkuu, Khartoum.

Uholanzi l OPCW, The Hague l Labortechniker

Netherlands l OPCW in The Hague l Mtaalamu wa maabara
Sudan yakanusha kutumia silaha za kemikaliPicha: John Thys/AFP

Mwezi Juni, Marekani iliweka vikwazo kwa serikali ya Sudan inayoshirikiana na jeshi kutokana na matumizi ya silaha za kemikali, lakini haikufafanua wapi na lini walizitumia.

Uchunguzi uliofanywa na Shirika la habari la France24, umeonyesha kuwa jeshi linaonekana kudondosha mapipa mawili yenye klorini Septemba 2024 karibu na kiwanda cha mafuta cha Al-Jaili kaskazini mwa Khartoum.

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Human Rights Watch limesema matumizi ya kemikali ya viwandani kama silaha, yanasababisha hali ya wasiwasi.

Sudan imerudia kukanusha madai ya Marekani, ikiyaita ''yasiyo na msingi'' na ''kitisho cha kisiasa''.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW