1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMyanmar

Ripoti: Kampuni za kigeni zaisaidia Myanmar kwa silaha

16 Januari 2023

Ripoti iliyotolewa na baraza maalaum la ushauri kwa Myanmar imesema kuwa kampuni kutoka takriban nchi 13 zimeisaidia nchi hiyo kujenga uwezo wake wa kutengeza silaha zinazotumika kufanya ukatili

Myanmar Naypyitaw | Militärparade
Picha: Aung Shine Oo/AP/picture alliance

Ripoti hiyo ya wataalamu huru wa kimataifa, imeelezea jinsi Myanmar ilivyoimarisha utengezaji wa silaha tangu jeshi kuchukuwa mamlaka kwa kutumia nguvu mnamo Februari Mosi mwaka 2021 na kuzua harakati za upinzani kutoka kwa umma. Ripoti hiyo imeendelea kusema kuwa kampuni za Marekani, Ulaya, Asia na Mashariki ya Kati, zinaendelea kuunga mkono usambazaji wa silaha za kijeshi na kuzitaka kampuni hizo kuhakikisha hazichangii katika ukiukwaji wa haki za binadamu.

Ukuaji wa kampuni za mataifa za utengezaji wa ndani wa silaha hutokea wakati mataifa mengine yamewekewa vikwazo vya silaha ama vikwazo dhidi ya watu binafsi na kampuni zilizohusika katika biashara ama utengenezaji wa silaha.

Marekani iliweka vikwazo

Mnamo mwezi Oktoba, wizara ya fedha ya Marekani iliweka vikwazo dhidi ya Aung Moe Myint, mfanyabiashara mwenye ushirikiano wa karibu na jeshi ambaye ripoti hiyo imesema anafadhili mikataba ya silaha kwa niaba ya jeshi hilo. Kakake, Hlaing Moe Myint pamoja na kampuni ya biashara walioanzisha ya Dynasty International pia alilengwa . Mmoja wa wakurugenzi wa kampuni hiyo Myo Thitsar, pia aliorodheshwa kuwekewa vikwazo.

Jeshi la MyanmarPicha: Aung Shine Oo/AP/picture alliance

Ripoti hiyo, imesema kuwa Myanmar haina watengenezaji silaha wa kibinafsi, kwa hivyo kampuni zozote kama hizo zinaendeshwa na wizara ya ulinzi.

Katika taarifa, mtaalamu wa baraza hilo la ushauri Chris Sidoti ambaye pia ni wakili wa kutetea haki za binadamu na mwanachama wa ujumbe wa uchunguzi wa Umoja wa Mataifa kuhusu Myanmar kutoka mwaka 2017 hadi 2019, alizihimiza serikali kufanya uchunguzi, na zinaporidhishwa, kuchukua hatua dhidi ya kampuni ambazo zinawezesha jeshi la Myanmar kutengeneza silaha zinazotumika kufanya mashambulizi ya kiholela dhidi ya raia. Sidoti ameongeza kuwa kampuni za kigeni zinazojipatia faida kutokana na mateso ya watu wa Myanmar lazima ziwajibishwe.

Kampuni za nje zinazoisaidia Myanmar kwa silaha

Ripoti iliyotolewa mwaka jana na Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, ilitaja baadhi ya kampuni kama hizo kutoka Urusi, China, Ukraine, Israel, Singapore na Ufilipino.

Sababu kuu inayosababisha kuongezeka kwa kampuni za ndani za kutengeza silaha ni hatari kwamba uagizaji silaha kutoka nje, ndege za kivita na silaha nyingine, huenda utakatizwa na vikwazo. Ripoti hiyo imesema kwamba jeshi sasa linajitegemea katika utengenezaji wa silaha ndogo ndogo.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW