1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Wanajeshi laki 5 wameuwawa au kujeruhiwa Ukraine

19 Agosti 2023

Takribani wanajeshi nusu milioni kutoka kila upande huenda wameuawa au wamejeruhiwa katika vita vinavyoendelea vya Ukraine.

Ukraine-Krieg I Donetsk
Picha: Libkos/AP/picture alliance

Takwimu hizo zimetolewa na gazeti la The New York Times ambalo limenukuu maafisa kutoka serikali ya Marekani.

Maafisa hao pia wameonya kwamba ni vigumu kukadiria madhara kamili yaliyojitokeza kwasababu Ukraine haichapishi takwimu huku Moscow ikishukiwa kuripoti takwimu za chini zinazohusu vifo na majeruhi.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, maafisa wa Marekani ambao hawakutajwa majina wanakadiria kwamba wanajeshi wapatao 120,000 wameuawa na kati ya 160,000 hadi 180,000 wamejeruhiwa upande wa Urusi.

Ripoti hiyo pia inaeleza kwamba wanajeshi 70,000 wameuawa na kati ya 100,000 na 120,000 wamejeruhiwa upande wa Ukraine.

Kulingana na New York Times, idadi hiyo inaweza kuongezeka maradufu wakati wa kipindi kinachokuja cha majira ya baridi na machipuko.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW