1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripoti kuhusu hali ya umaskini nchini

Hamidou, Oumilkher19 Mei 2008

Hali ya umaskini yatishia hata watu wa tabaka ya kati

Waziri wa misaada ya maendeleo Wieczorek-Zeul akutana na Dalai LamaPicha: picture-alliance/ dpa


Wahariri wamejishughulisha zaidi hii leo na ripoti mpya ya serikali kuhusu umaskini.Mada nyengine magazetini ni kuhusu mvutano ndani ya chama cha Social Democratic-SPD kuhusu ziara ya Dalai Lama.


Tuanze basi na ripoti ya serikali inayotazamiwa kutangazwa rasmi hii leo kuhusu hali ya umaskini humu nchini .Gazeti la FRANKFURTER RUNDSCHAU linaandika:



Pengo kati ya waalio juu na wale walioko chini linazidi kupanuka.Na idadi ya wale wanaokabiliwa na kitisho cha kuporomoka, inaongezeka.Yadhihirika kana kwamba kundi la wale ambao mwishoni mwa mwezi,katarasi za mishahara hazisaidii kitu linazidi kua kubwa.Kwa maneno mengine kazi sio kinga.Ni kifimbo cheza hiki kinachoashiria mivutano ya kisiasa.Kinawapatia hoja wasocial Democrat wanaopigania mshahara wa kima cha chini,wana CSU wanaotaka kodi ya mapato ipunguzwe,shirikisho la vyama vya wafanyakazi DGB wanaodai malipo ya walala hoi wa muda mrefu yazidishwe na wafuasi wa mrengo wa shoto wanaodai asili mia 50 ya kodi ya mapato kwa matajiri.Ripoti kuhusu hali ya umasikini hairuhusu siasa ya aina moja,linamaliza kuandika FRANKFURTER RUNDSCHAU.


Gazeti la MÄRKISCHE ODERZEITUNG la mji wa Frankfurt katika jimbo la Brandemburg linahisi:


"Ukuta hauitenganishi pekee mashariki na magharibi,unawagawa pia wenye nacho na wanaotegemea,waajiriwa na walalahoi,na kuwatenganisha wasomi na wasioelimika.Kwa wengi umaskini ni tukio la muda.Lakini kwa wale ambao hawamudu kujikomboa,serikali inabidi iingilie kati.Kwa miradi gani,kiwango gani cha fedha na juhudi za aina gani ,masuala yote hayo yanabidi kuwatia mbioni wanasiasa wanaobishana juu ya tarakimu zilizotajwa andani ya ripoti hiyo kuhusu hali ya umaskini miongoni mwa jamii.


Katika wakati ambapo WESTDEUTSCHE ZEITUNG linashuku mikakati ya kupambana na umaskini gazeti la SÄCHSISCHE ZEITUNG linatoa pendekezo jengine na kuandika:


" Masomo na mafunzo ya kazi ndio njia pekee bora ya kupambana na umaskini.Misaada zaidi kwa familia,mama au baba anaelea peke yake watoto wake,njia bora za kuwahudumia watoto na utaratibu bora wa kuwashughulikia vijana wanaokabiliwa na hatari ya kufuata mguu mbaya wanapokua shuleni,inaweza kuimarisha haki sawa kwa wote,ili kila mmoja aweze kujipatia kazi,hata kama haitamtajirisha lakini angalao itampatia mshahara unaokidhi mahitaji yake.


Mada ya pili magazetini ni kuhusu mvutano ndani ya chama cha SPD kuhusu mazungumzo anayopanga kua nayo waziri wa misaada ya maendeleo bibi Heidemarie Wieczorek-Zeul n kiongoi wa kiroho wa Tibet Dalai Lama.Gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG linaandika:


"Katika wakati ambapo wanasiasa wa CDU/CSU wanakutana bila ya shida yoyote pamoja na mgeni huyo wa kutoka Tibet,katika chama cha SPD wanasiasa wanazozana kama kuna haja kweli ya kukutana na kiongozi huyo wa kiroho,miezi michache kabla ya michezo ya Olympik kuanza mjini Beijing.Mwenyekiti wa chama cha SPD Kurt Beck amelalamika sana kwa kushindwa kuzuwia mazungumzo yasifanyike kati ya Dalai Lama na waziri wa misaada ya maendeleo Heidemarie Wieczorek-Zeul.Ni aibu kubwa hii kwa chama ambacho wakati wote kimekua kikijifungamanisha na wapenda amani,uhuru na demokrasia.Ni aibu kwa Ujerumani nzima pia.Kwasababu wananchi wanaiangalia mizozano kuhusu Dalai Lama kua si chochote chengine isipokua mbinu za kutaka kuiridhisha China tuu.